Monday, September 24, 2007

WASOMI WANAOGOPEKA?

Ninalazimiza kujiuliza swali “wasomiwanaogopeka?” kutokana na sababu mbalimbali.Sababu ya kwanza kwa mfano kama unaomba kazi,kama kwa bahati mbaya una shahada(wanaiita dgirii) moja tayari ni matatizo.Utaandika barua nyingi sana wakati wa kuomba kazi na nyingi sana hazitajibiwa kisa wanaogopa wasomi!
Sio Kwamba huna sifa zinazostahili bali ni kwamba ni “tishio” kwa nafasi ambazo watu wameshaziwekea booking tangu enzi na enzi!Utaingia kazini kama umebahatika kupata nafasi ya kazi utakutana na vimbwanga vingine.Kwanza kila mtu atajiweka kando aone utafanyaje!Siku hizi wanita wtoto wa kikwete(ari mpya na kasi mpya)Hata ukienda baa au kijiweni watajiweka kando kabisa!Mbaya zaidi mtu anaweza kukuuliza hivi kwa nini umekuja hapa kupoteza muda?Hivi watu waende wapi?wakafanye kazi wapi?Kwa nini watu waliosoma wanogopeka kiasi hiki?

Hiyo ni Shahada ya Kwanza,Itakuwa hatari sana sana kwa mfano kama umeajiriwa kwenye ngazi kwa mfano wilayani ukiwa na shahada ya pili(wanaita Masters au Mastaa) kwani utapata wakati mgumu sana mpaka uweze kuzoeana na wafanyakazi wengine.
Sisi watanzania tunasoma ili tuweze kuisaidia jamii yetu kwa kutumia ujuzi ambao tumeupata.Kichekesho kinakuwa pale unapoambiwa eti kwa nini hukubaki mjini au kwa nini hukutafuta kazi kubwa?Hii inatokana na dhana mbaya inayojengeka katika jamii kwamba mtu akishapata shahada ya kwanza au diploma ya juu basi hatakiwi kuwa karibu tena na watu wa kawaida!hii nadhani ni dhana ambayo si sahihi kabisa!

wasomi wanaogopeka mno!

2 comments:

Sharifu said...

Ndugu yangu mbona blogu umeitelekeza? Pita hapa kwangu tuelekezane kidogo

Sharifu said...

Ndugu yangu mbona blogu umeitelekeza? Pita hapa kwangu tuelekezane kidogo